KANUNI AU TABIA ZA MJASIRIAMALI

TABIA  AU SIFAZA UJASIRIAMALI.

Ni tabia gani unahitaji ili upate mafanikio katika biashara au shuguri yoyote unayofanya?

ili ufanikiwe katika shughuri au biashara unayofanya au unayotarajia kufanya ni lazima uwe na mtazamo sahihi na mtazamo chanya. ujasiriamali una kanuni zake amboazo ni muhimu sana ili mtu afikie mafanikio aliyoya panga,kama mtu akishindwa kufuata kanuni hizo basi anakuwa na nafasi ndogo ya kupata mafanikio katika shughuri yake. 

KANUNI ZA UJASIRIAMALI

Tabia za ujasiriamali zinaweza kusomwa au kufundishwa na mtu akaelewa na kuzifuata,lakini  tabia  zingine  hazifundishiki hizi ni zile tabia ambazo mtu anazaliwa nazo. Kila binadamu anauwezo tofauti katika kufikili,kufanya maamuzi,kufanya kazi kwa bidii,tofauti hizi ndizo ambazo haziwezi kufundishika. Jambo la kutia moyo ni kwamba tabia ambazo zinafundishika ni muhimu sana kwa mjasiriamali au mtu yeyote anayetaka kufanikiwa katika biashara. Zifuatazo ni tabia za ujasiriamali.
1.       kuthubutu
hii ni tabia muhimu sana kwa mjasiriamali,hapa tunazungumzia uwezo na utayali wa kufanya maamuzi ya kuingia katika biashara fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara,mradi n.k,watu wanaogopa hasara,hawajui jinsi ya kuendesha amradi weyewe. Mtu ili aitwe mjasiliamali ni lazima awe na uwezo wa kuhtubutu kufanya jambo, lakini jambo atakalo thubutu kufanya lazima afanye utafiti wa kutosha il baadaye limletee tija. Waswahili mwanasema” UWOGA NI UMASIKUNI”.
2.       Nidhamu
Hii pia ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali,mjasiriamali lazima awena na nidhamu katika biashara yake,awe na nidhamu katika matumiza yake ya pesa na ni lazima awe na nidhamu ya kufanya kakazi kwa bidii.nidhamu ni hanzo ch mafanikiao. Mfano mfanyabiashara wa duka ni lazima uwe na nidhamu kwa wateja wake ili awasimkimbie.
3.       Umakini na uelevu
Wale waliofanikiwa sio tu walikuwa tayari kufanya akazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi waliyokuwa wakifanya. Mjasiriamali anatakiwa kuwa makini kwa kila jambo,anatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe muelevu wa kutambua mabadiriko yanayojitokeza katika soko ,uzalishaji na uendeshaji kwa ujumla.
4.       kuwa na uwezo wa kuongoza
mjasiriamalia lazima awe na uwezo wa kuongoza na kutoa maamuzi. Baadhi ya watu wanadai uongozi  ni kalama ombayo mtu anazaliwa nayo au anapewa na Mungu,ni kweli mtu anaweza kuzaliwa na kipaji cha kuongoza,lakini mtu anaweza kujifunza na akawa kiongozi mzuri. Katika ujasiliamali uongozi ni jambo muhimu sana,mjasiliamli lazima aweze kuogoza biashara yake au mradi wake vizuri. Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kusimamia wafanyakazi na kutumia mbinu  za uogozi ili apate matunda kwaklile ambacho anafanya.
5.       Kupenda kufanya kazi (kufanya kazi kwa bidii na maarifa)
Kitu kikubwa  hapa ni lazima mjasiriamli awe anaipenda kwa dhati shughuri anayofanya hii itamasahidia kufanya kazi kwa moyo.Kama unapenda kazi unayo fanya basi kaziyo haitakuwa mgumu bali,bali utakuwa unafanya kitu ambacho kwa ko ni hobi na mwisho wa siku utafanya kazi kwa bidii na amaarifa. Watu waliofanikiwa ni wachapakazi.hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya kufanya kazi kwa bidii.
6.       Uaminifu na ukweli
Hii nayo ni tabia ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwanayo,watja wengi wanapenda mtu mwamifu na mkwali. Kama mjasiriamali ni lazima ufanye kazi yako katika mazingira ya uamifu na ukweli ili upate wateja wengi,lazima uwe mkweli katika bei  zako. Uongo katika biashara ni sumu ambayo itaua biashara yako.
7.       Dhamira
Mtu yeyote naweza kujiita mjasiriamali lakini kiukweli mafanikio yanahitaji uelewa wa kutosha,kufanya kazi kwa didii huku ukiwa umeweka mbele lengo au dhaira. Lengo au dhamila ni motisha tosha itakaoyo kupa msukumo mpaka kufikia mafanikio. Dhamira ya kweli inahijajika kabla hujaingia katika biashara au mradi fulani.
8.       Kwenda na wakati
Mjasiriamali lazima aende na wakati iliaweze kutambua mabadiriko mbalimbali yanayo jitokeza katika masoko na uzalishaji wa bidhaa kwa ujumla. Kwenda na wakati hakutampa nafasi mjasiriamaili kuachwa nyuma katika ushindani wa kibiashara katika soko huria,kwenda na wakati pia kunatoa fulsa kwa mjasiriamali kujua njia mpya za uzalishaji. Njia ambazo zinaweza kukusaidia kwenda na wakati ni pamoja na kusoma magazeti,kufanya utafiti,kurambaza katika mitandao mbalimbali.

Tabia ambazao zimeorodheswa hapo juu ni tabia za ujumla ambazo mjasiriamali anatakiwa kuwa nazo,lakini kama huna baadhi ya tabia hizo usifadhaike kwani ujasiriamalia ni somo na sio kipaji.








14 comments:

  1. Nimeipenda sana, big up kaka!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thanks sana,tupeane hamasa ili tufanikiwe katka haya maisha..

      Delete
    2. This comment has been removed by the author.

      Delete
  2. Jaribu kufanya uhariri kwenye makala zako. Najua Kiswahili sio lugha mama yako. Kama wewe huwezi, wape wanaoijua vema lugha hii wazifanyie kazi makala zako, ili ziweze kueleweka vizuri. PRESENTATION! PRESENTATION! PRESENTATION!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka nimekuelewa sana na nashukuru kwa kutoa mapungufu yangu..nitajirekebisha ili niweze andika makala bora zaid,nahitaji wakosoaji ili nifanye kitu bora..

      Delete
  3. nimepata kitu kitanisaidia katika harakati zangu za kiujasiriamali

    ReplyDelete
  4. ukweli ni kwaba ujumbe unaokusudiwa na mwandishi kwa wasoaji wake hakika umefika na ni wafaida kwetu sisi tunaoanza biashara au ujasiriamali ila boresha au pitia mara mbili makala yako kabla haujaipost ili kurekebisha makosa dhahiri ya kiuandishi na maneno sanifu ya sarufi na kimaana ya kiswahili.

    ReplyDelete
  5. Asante sana kwa kunipa mwanzo nzuri wa ninachotaraji kukifanya maishani mwangu

    ReplyDelete