ujasiriamali kama kazi
Nimesha eleza sana juu ya dhana
ya ujasiliamali katika blog(gjobu.blogsport.com) hii hivyo si vizuri nikirudia.
Ujasiliamali kama kazi hapa nalenga kuonyesha ni jinsi gani mtu anaweza
kujiajiri kama mjasiliamali na kuachana na mawazo ya kuajiriwa. Kuwa na mtaji
peke haitoshi ili mtu aweze kujiajiri bali mjasiliamali anahitaji kujua na
kuvifanyia kazi vitu vifuatavyo ambavyo ni jinsi ya kupata wazo la
biashara,kugundua na kutambua biashara sahihi,vigezo muhimu wakati wa kuchagua
biahara ya kufanya,vitu muhimu vya kufuata wakati wa kuanzisha biashara na kazi
za mjasiliamali.
Kabla hujanzisha biashara jiulize maswali yafuatayo
- Kwanini unataka kuanzisha biashara?
- Je upo tayari kufanya biashara?
- Je unamalengo gani katika biashara hiyo?
- Je unaujuzi na elimu ya kutosha katika kunzisha,kuendesha na kukua kibiashara?
- Mtaji kiasi gani unahitajika ili kuanzisha biashara?
- Biashara ya pekeyako au ya ushirikiano?
Jinsi ya kupata wazo la biashara
- Tafuta msaada toka kwa wote ambao wapo katika
biashara,watakwambia vitu muhimu katika biashara.
- Angalia wengine wanafanya nini, tambua matatizo
wanayokumbana nayo na kisha fikiri njia sahihi za kutatua matatizo hayo.
- Jadiri pamoja na marafiki na jamaa wa karibu juu
ya kile unchotaka kufanya
- Kuwa mdadisi kwa kuchunguza vitu kwa
makini,tembelea maeneo mengine ili kujua wanafanya nini
- Fikiri kufanya kiu kipya ambacho hakijafanywa
katika eneo ulilopo
Faida za kuwa na wazo la biashara
- Hupunguza vikwaazo katika kuendesha biashara
- Husaidia katika kufanya maamuzi sahihi ya
biashara gani uanzishe\
- Kupata mafanikia katika biashara
- Ni hamasa kubwa katika kuingia katika biashara
Jinsi kuugundua na kutambua biashara sahihi
- Kuwa makini katika kuchaga aina ya biashara ya
kufanya
- chagua kulingana na uwezo wako katika kuendesha
biashara hiyo
- chagua biashara unayo ipenda kwani uwezekano wa
kuifanya vizuri ni mkubwa
- amua biashara ya kufanya hasa bada ya kufanya
uchunguzi wa kutosha na kutafuta habari za kina juu ya biashara husika hi
itakusaidia kufanya biashara bilia vikwazo vingi
vigezo muhimu wakati wa kuchagua biashara ya kufanya
v
uwezekao a kufanikiwa
v
kupata faida
v
kutambua vikwazo katika bishara
v
biashara inayo vutia
v
elimu ya biashara pamoja na rasilimali watu
v
mtaji
v
masoko
v
upatikanaji wa stoo za kuhifadhia bidhaa
v
upatikanaji wa malighafi
v
usafiri
v
uwezekano wa kupata msaada toka serikalini
kazi ya mjasiliamali
- kuaandaa mpango wa biashara
- kuatafuta mtaji
- kupanga bei
- kutunza kumbukumbu za biashara
- kutunza fedha
- kujitegemea
- kuchanganua gharama
- kutangaz bidhaa anazouza
- kubaini vikwazo katika biashara
- ubunifu
Ufunguo wa
mafanikio katika ujasiliamali
mpango biashara
kabla hujaanza biashara hakikisha unaandaa/kuandika mpango
biashara madhubuti ambao utaeleza kipi utafanya na mpangilio mzima wa biashara
yako. Pia fikiri kuhusu kesho, wiki ijayo na tazama mbele zaidi
dondo
- tambua mambo yanaenda yakibadirika hivyo nawe badirika kulinga ana wakati pomoja na mazingira
- tambua kuwa huwezi fanya kila kitu pekeyako
- mjasiliamali mzuri ni yule anaye fikiri na kutazama mbele (future oriented)
- mjasiria mali mzuri ni yule anayetumia muda vizuri
- mpango biashara utakusidia kuona fulsa mpya na chagamoto mbalimbali katika biashara zako
- tafuta ushauri toka kwa wataalamu mbalimbali wa biashara na ujasiliamali kwa kile unacho kifanya
- uthubutu ni ufunguo wa mafanikio katika ujasiliamali.
Jinsi ya kupata mafanikio katika biashara
Kunanjia nyigi unaweza kuzitumia ili kufikia mafanikio
katiaka biashara baadhi ni kama zifuatazo.
Fikiri kuhusu……
- jinsi ya kubadiri wazo la biashara na kuwa
biashara
- imarisha na ongeza ubora wa bidhaa na huduma
unazotoa
- gundua,tambua na anzisha bidhaa mpya na huduma
- vutia wateja
- simamia biashara yako hata kama haupo (weka
wasaidizi)
- ongeza juhudi
- ajiri wasaidizi bora
jitofautishe katika utoaji wa huduma na bidhaa
kwanini wateja waje kwako?
Kujitofautisha katika kuuza bidhaa na aina ya huduma
unayotoa ni kitu muhimu hii itasababisha wateja weni wafuate huduma
zako,wafanya biashara wengi wanaamini kuwa kupunguza bei ni kivutio kikubwa cha
wateja katika biashara, lakini sio bei tu ianayo weza kuvutia wateja wengi
katika huduma zako, wateja wengi huthamini huduma bora na bidhaa bora kama
ifuatavyo….
- Ubora wa bidhaa yenyewe nahduma unazo toa
- Urahisi wakupata huduma na bidhaa zako
- Upatikanaji wa bidhaa na huduma (je zina patikana muda wote?)
- Usalama wa bidhaa na huduma zako
- Je bidhaa au huduma zako haziharibu mazingira
- Bidhaa zako zimezalishwa wapi?......nchini au ughaibuni.
- Maoni ya wateja wako juu ya bidhaa na huduma unazotoa, wanasemje juu ya bidhaa na huduma zako
- Kilasiku buni na fikiri njia mbali mbali ambazo zitafanya wateja apende bidhaa zako zaidi.
👊👊
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteje unataka kusoma,kutimiza malego
ReplyDeletekama kujenga nyumba kununua gari au unatafuta
ajira na ungependa kupata msaada.
tunatoa usaidizi katika yote haya. bila hati ya nyumba au ya gari utaweza kupata mkopo usiokuwa na riba.karibu sana
BONYEZA link http://4ui.us/pataunachotaka Kwa taarifa za kina.
This comment has been removed by the author.
Delete