JINSI YA KUPATA MTAJI NA NAMNA YA KUTUMIA MTAJI KATIKA BIASHARA

MTAJI

Mtaji ni kitu chochote ambacho unaweza kutumia katika kuzalisha kitu kingine kwa lengo la kupata faida.Biashara oyote iwayo lazima ianze na mtaji. Kuna aina tano za mitaji kama ifuatavyo:-

1. Mtaji wa fedha( financial capital)

2. binadamu mwenyewe( human capital) vitu kama ujuzi, elimu na kufanya kazi kwa bidii.

3. Jamii ( social network capital) ushirikiano na watu wengine katika biashara

4. utamaduni halisi wa mjasiliamali- utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii,historia ya familia

5. fani au utaalamu  katika jambo flani

JINSI YA KUPATA MTAJI.

hapa tunaangalia vyanzo vya mtaji kwa mjasiliamali. Wajasiliamali wengi wanapata changamoto kubwa katika kupata mitaji ya kuanzishia biashara. nivigumu kuanzisha biashara bila kuwa na mtaji wa kutosha,hivyo basi mtaji ni muhimu sana lakini mtaji pekeyake hautoshi kuanzisha biashara ni lazima uwe na elimu ya ujasiliamali ili uweze kufanikiwa katika biashara. kuna njia mbalimbali za kupata mtaji na njia hizo zimegawanyika katika mafungu mawili ambayo ni chanzo cha ndani na chanzo cha nje.

Chanzo cha ndani ( internal sources of capital)

1. Mtaji   toka kwa mjasiliamali mwenyewe. huu ni mtaji ambao mjasiliamali anakuwanao kabla hajaanza biashara. huu ni mtaji bora sana kwani humilikiwa na mjasiliamali mwenyewe na hatakiwi kurudisha rejesho hata baada ya kupata faida.

2. Mtaji ambao unapatikana wakati biashara injiendesha. faida inayopatikana katika biashara inaweza kutumika kama mtaji. njia hii ndio huchangia kukua kwa biashara.

3. hisa. baadhi yawajasiliamali wanaweza kuamua kuwekeza katika hisa za makampuni. uwekezaji katika hisa husaidia kupata mtaji pale ambapo kampuni litagawa faida kwa wanachama waliowekeza katika hisa. pia mjasiliamali anaweza kupata mtaji kwa kuuza hisa kwa mtu mwingine au muwekezaji wa nje.

chanzo cha nje ( external sources of capital)

hapa tunaangalia mtajia ambao mjasiliamali anaweza kuupata toka nje ya yeye mwenyewe. baadhi ya vyanzo    hivyo ni kama ifuatavyo.

1. mkopo toka benki
huu ni mkopo ambao ulipaji wake ni wa muda mrefu.viwango vyariba si vikubwa sana ambavyo mjasiliamali anaweza kumudu kulipa endapo biashara itafanikiwa. mikopo ya benki inahitaji dhamana ya vitu visivyo hamishika mfano nyumba, shamba nk. 




  

18 comments:

  1. Mm sina elimu yoyote ya biashara/ujasiliamali je ntwezaje kuanzisha biahsara zangu na mda huo huo nahitaji pesa yangu izae na isikaaee tu kama mawe!.

    ReplyDelete
  2. watu wengi tuna mawazo ya kuwa wajasiria mali tatzo ni mitaji na ukienda bank masharti ni mengi san na magumu tunashindwa kukidhi vigezo

    ReplyDelete
  3. Mi Naitwa Erick Kiwelu Nimechukua Mafunzo Ya Ujasiriamali Na Kuhitimu Na Kupata Cheti Ila Tatizo Ni Mtaji Naombeni Mnikopeshe Sh, Laki Mbili Na Nusu Namba Yangu Ni 0719353919 Kwa Yoyote Atakayenisaidia Huo Mtaji Ntamshukuru Sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu nimepita mtandaoni nmekuta makala ya wazo lako la kuombaba mtaji sh lak 2 planning yako ni Nini ukipata hiyo hela tushare mawazo please

      Delete
  4. hakika ni kweli ila ukiws huna vyote hivyo ni ngumu kuwa mjasiliamali

    ReplyDelete
  5. WAZO LAKO LA KUFANYA BIASHARA PIA NI MTAJI .KAMA UNA WAZO KUWA NA SUBILA NA MALENGO MUNGU ATAKUSAIDIA UTAANZA BIASHARA

    ReplyDelete
  6. Ukiwa na mtaji hakuna kinachoshindokana

    ReplyDelete
  7. ndg zangu vijanaa wengi tunashindwa kutimiza ndoto zetu kwa sababu ya pesa ya mtaji atuna me naomba yyte mweny uwezo wa kunisaidia mtaj naomb tuwasiliane kwa no 0689065586

    ReplyDelete
  8. Wengi mawazo mazuri ya biashara tunayo shida IPO kwenye mtaji

    ReplyDelete
  9. Habari mm ni mjasilia mali nauza karanga , ubuyu, pamoja na korosho nawezaje kupata elimu ya usindikaji bora wa bidhaa zaangu na kuhikuza kiwiraya kimikoa na kimataifa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wasiliana nasi tutakusaidia na hata kuweza kumiliki kiwanda cha kusindika Korosho na vyakula vingine mbalimbali.

      Kumbuka, sisi tunatengeneza mashine za kuchakata na kusindika vyakula mbalimbal8, kilimo na ufugaji, mashine za ujenzi, n.k

      Namba zetu in 0682 836 463

      Hii ni kwa yeyote mwenye uhitaji wq mafunzo ya usindikaji vyakula na mashine

      Delete
  10. Mm pia mjasiliamali ila tatzo mtaji hakuna

    ReplyDelete
  11. Mi Nina wazo la biashara mwenye pesa Ila Hana wazo aje tubadilishane

    ReplyDelete